Inajuzu kwa mfungaji kumbusu mke wake na kucheza nae?


Swali: Inajuzu kupaka hina kwenye nywele wakati wa kufunga na wa kuswali? Nimesikia kuwa hina inafunguza?

Jibu: Hili halina usahihi wowote. Kupaka hina wakati mtu amefunga hakufunguzi na wala haiathiri swawm kitu. Ni kama kupaka wanja, kuweka tone kwenye masikio na kwenye macho. Yote hayo hayadhuru na wala hayamfunguzi mfungaji.

Ama kupaka hina katikati ya swalah sielewi anachomaanisha. Kwa sababu mtu ambaye anaswali hawezi akapaka hina. Pengine anamaanisha kama hina inazuia kusihi kwa wudhuu´ ikiwa mwanamke amejipaka hina? Hilo halizui kusihi kwa wudhuu´. Hina haizuii kufika kwa maji. Hina ni rangi peke yake. Kile kitu kinachozuia maji yasiufikie mwili ndicho ambacho kinatakiwa kuondoshwa ili wudhuu´ uweze kusihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/227)
  • Imechapishwa: 12/06/2017