Inajuzu kwa anayesafiri 1,472 km na ndege kuacha kufunga Ramadhaan?

Swali: Inajuzu kwa ambaye anasafiri na ndege kutoka ar-Riyaadh kwenda Cairo kuacha kufunga Ramadhaan?

Jibu: Kuacha kufunga safarini ni mlango wa ruhusa, wepesi wa Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa waja wake na kuwaondoshea ule uzito wanaopata. Kuzitendea kazi ruhusa za Allaah ni jambo linapendwa na Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Allaah anapenda ruhusa Zake zitendewa kazi kama anavyochukia kuendewa maasi. Kwa hivyo kwa mfano mtu anasafiri kuelekea Cairo katika Ramadhaan inafaa kwake kuacha kufunga. Endapo atafunga basi swawm yake ni sahihi.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/205)
  • Imechapishwa: 06/06/2017