Swali: Mimi naishi na ndugu zangu ambao hawaswali na mimi ninawapenda sana na wala siwezi kutengana nao kwa kuwa sina wengine badala yao. Je, inajuzu kuishi nao?

Jibu: Ikiwa haswali hutakikani kuwapenda na wala hulazimiki kuwa na mapenzi juu yao kwa ajili ya Allaah, kwa kuwa watu hawa udhahiri wao ni ukafiri. Kwa kuwa mwenye kuacha Swalah anakufuru. Hivyo, ilikuwa haitakikani kuwapenda, bali uwachukie kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na wala hutakiwi kuishi nao. Isipokuwa tu ikiwa kama ni jambo la kidharurah, hivyo utawanasihi daima, na kuwaogopesha Allaah, na kuwaambia “muogopeni Allaah enyi watu, swalini, zihifadhini Swalah, mcheni Allaah”. Saidiana na aliye karibu yako katika ndugu zako; kama baba zao, babu zao, mama zao na mfano wa hao mpaka waweze kukusaidia[1] katika kuwapa nasaha na kuwaelekeza katika kheri. Wakiendelea kuacha Swalah, watu hawa watakuwa hawana kheri yoyote. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa kasema: “Ahadi iliopo baina yetu na wao ni Swalah, atakayeicha basi amekufuru.” Fanya vovyote utavyoweza usiishi nao, hata ikibidi kuishi katika nyumba ya wewe mwenyewe au baadhi ya ndugu zao wengine fanya hivyo. Hili ndilo la wajibu kwako kadiri na utakavyoweza.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/jirani-kafiri-ambaye-haswali-hatakiwi-kusaidiwa/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 30/03/2018