Inajuzu kutoa Zakaat-ul-Fitwr kabla ya ´iyd?

Swali: Inajuzu kutoa Zakaat-ul-Fitwr kabla ya ´iyd?

Jibu: Inajuzu kutoa Zakaat-ul-Fitwr siku moja au mbili kabla ya ´iyd. Bora ni kuitoa ile siku ya ´iyd kabla ya kuswali ´iyd. Haijuzu kuichelewesha kuitoa mpaka wakati wa kuswaliwa ´iyd. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha Zakaat-ul-Fitwr itolewe kabla ya watu kutoka kwenda kuswali ´iyd.”

Katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuitoa kabla ya swalah, hiyo ndio zakaah yenye kukubaliwa, na yule mwenye kuitoa baada ya swalah, hiyo ni swadaqah miongoni mwa swadaqah.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/267-268)
  • Imechapishwa: 23/06/2017