Inajuzu kuswali kwenye msikiti uliojengwa kwa mali ya haramu?

Swali: Ipi hukumu ya kuswali ndani ya msikiti ambao umejengwa na bwana mmoja ambaye mali yake sehemu yake kubwa ni kutokana na haramu? Je, hukumu yake ni kama kuswali katika ardhi ambayo imeporwa? Kama hukumu si moja afanye nini?

Jibu: Misikiti iliyojengwa kwa mali ya haramu au kwa mali ilio na haramu hakuna neno kuswali ndani yake na wala hukumu yake si kama ya kuswali kwenye ardhi ilioporwa. Kwa sababu mali ambayo ndani yake mna haramu au yote ni kutokana na haramu mali hiyo inatolewa katika miradi ya kidini. Wala mali hiyo haichwi wala kuchomwa moto. Bali ni lazima kuitoa katika miradi ya kidini. Kama kwa mfano kuwapa swadaqah mafukara, kujenga misikiti, kujenga vyoo, kuwasaidia Mujaahiduun, kujenga daraja na vyenginevyo katika manufaa ya waislamu. Mali hiyo haina hukumu ya kuporwa. Kwa sababu uporaji ni mali iliochukuliwa kimabavu na kwa dhuluma. Ama kuhusu watu hawa wameingiliwa na mali kutoka katika njia ambazo hazikubaliki Kishari´ah.

Kwa hivyo ni lazima kwao kuitoa katika njia za dini pamoja na kutubia kwa Allaah kutokamana na kitendo hicho. Mali iliotolewa katika njia kama hizi za kidini inakuwa mwenye nayo amesalimika kutokamana na madhara pamoja na kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Jengine ni kwamba mali hiyo inakuwa ni yenye kuwanufaisha wailsamu badala ya kuiharibu na kuichoma moto.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/13788/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D9%85%D8%B3%D8%AC%D8%AF-%D8%A8%D9%86%D9%8A-%D9%85%D9%86-%D9%85%D8%A7%D9%84-%D8%A7%D9%83%D8%AB%D8%B1%D9%87-%D9%85%D9%86-%D8%AD%D8%B1%D8%A7%D9%85
  • Imechapishwa: 18/01/2020