Inajuzu kupokea malipo kwa ajili ya adhaana?

Swali: Inajuzu kupokea malipo kwa sababu ya kutoa adhaana?

Jibu: Haijuzu kuchukua malipo kutoka kwa mtu. Hata hivyo inafaa kuchukua malipo kutoka katika nyumba ya mali ilioko kwa ajili ya manufaa ya waislamu. Lakini haijuzu kushurutisha na kusema kuwa hauwezi kuadhini isipokuwa mpaka upewe malipo ya hilo. Hakutiliwi masharti katika ´ibaadah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 22/01/2017