Swali: Je, inajuzu kupamba misikiti?

Jibu: Hapana. Haikujengwa kwa ajili ya kupambwa. Imejengwa kwa ajili ya ´ibaadah. Malengo ni unyenyekevu na kumuogopa Allaah (´Azza wa Jall). Haikujengwa kwa malengo ya fakhari. Haikujengwa kwa ajili ya makumbusho. Waseme haya ni mabaki makubwa ya waislamu. Ni kweli ya kwamba misikiti ni mabaki ya waislamu, lakini hata hivyo haina maana ya kwamba inatakiwa kupambwa. Misikiti yote ni mikubwa hata kama haikupambwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tahid-25-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017