Inajuzu kuoa mwanamke ambaye niliwahi kumpa damu yangu?


Swali: Nimechumbia mwanamke wa umri wa miaka ishirini, na niliwahi kumsaidia kwa kumpa damu pindi alipokuwa mgonjwa kabla sijamchumbia. Je, inajuzu kwangu kumchumbia?

Jibu: Damu haiathiri, sio kama kunyonya. Mwanamke kuolewa na mwanaume ambaye ana damu yake, au mwanaume kuoa mwanamke ambaye ana damu yake aliyompa wakati wa haja ya hilo, hili halina hukumu kama ya kunyonya. Mwanamke haharamiki kwake (mwanaume) wala (mwanaume) haharamiki kwake (mwanamke) kwa yaliyopitika katika kunufaishana kwa damu ambayo anaihitajia mgonjwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 31/03/2018