Swali: Inajuzu kumdhukuru Allaah chooni?

Jibu: Haitakikani kwa mtu kumdhukuru Mola wake (´Azza wa Jall) ndani ya choo. Sehemu hii haistahiki. Hakuna neno endapo atamtaja kwa moyo wake pasi na kutamka kwa mdomo wake. Vinginevyo bora asitamke kwa mdomo wake katika sehemu kama hii na badala yake asubiri mpaka atapotoka.

Lakini ni sawa kumtaja Allaah ikiwa ni sehemu ya kutawadhia peke yake ambako kumetengana na sehemu ya kukidhia haja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/110)
  • Imechapishwa: 13/06/2017