Inajuzu kula na kunywa wakati wa adhaana ya alfajiri?

Swali: Inajuzu kula na kunywa katikati ya adhaana ya muadhini?

Jibu: Ikiwa muadhini anaadhini pale tu ambapo alfajiri inaingia, basi itakuwa haijuzu kula na kunywa pindi atakapoanza kuadhini. Ama ikiwa muadhini anaadhini kabla ya alfajiri ni sawa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Bilaal anaadhini usiku. Hivyo kuleni na kunyweni mpaka aadhini Ibn Umm Maktuum.”

Ibn Umm Maktuum alikuwa haadhini mpaka aambiwe: kumekucha. Kwa kuwa alikuwa ni mtu kipofu. Kwa hivyo alikuwa haadhini mpaka aambiwe kuwa kumekuja. Bi maana asubuhi imeanza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 30/05/2017