Inafaa mwanamke kujifunua mbele ya baba wa mume wa kunyonya?

Swali: Baba yangu wa kunyonya anazingatiwa ni Mahram kwa mke wangu? Ni kanuni ipi inayotumika katika unyonyaji?

Jibu: Wanachuoni wengi wanasema baba wa kunyonya ni kama baba wa mke kinasabu. Maoni sahihi kwangu naonelea tofauti na hivyo. Pia ndio chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah). Anaonelea kuwa baba wa kunyonya hana mahusiano yoyote na mke wake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yanaharamika kwa ajili ya kunyonya yale yanayoharamika kwa ajili ya nasabu.”

Baba wa mume huyo ni haramu kwa sababu ya hali ya ukwe sio kwa sababu ya nasabu. Kwa ajili hiyo tunaona kuwa si halali kwa mke wa mtoto wa baba wa kunyonya kujifunua mbele yake kwa sababu sio katika Mahram zake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/852
  • Imechapishwa: 24/04/2018