Inafaa kwa wote hawa wakajenga msikiti

Kuhusu kitendo cha ujenzi wa misikiti inafaa kujengwa na mwema, mtenda dhambi na kafiri. Kitendo hicho kinaitwa ´ujenzi`. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumjengea Allaah msikiti, basi Allaah atamjengea nyumba Peponi.”

Allaah amebainisha kwamba haiwapasi washirikina kuamirisha misikiti ya Allaah pamoja na kushuhudia juu ya nafsi zao ukafiri na pia akabainisha kuwa wenye kuiamirisha ni wale wenye kumwamini Allaah, siku ya mwisho, wakasimamisha swalah, wakatoa zakaah na hawamchi mwingine zaidi ya Allaah. Hizi ni sifa za wale watu wanaomwabudu na kumtakasia nia Allaah pekee ambao hawamchi mwingine isipokuwa Allaah, hawamtegemei mwingine zaidi Yake, hawamtaki msaada mwingine isipokuwa Yeye, hawamwombi mwingine isipokuwa Yeye.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/499)
  • Imechapishwa: 25/08/2020