Inafaa kwa mwenye nifasi kutoka nyumbani wakati wa eda?

Swali 148: Je, inafaa kwa mwanamke mwenye damu ya uzazi kutoka nje ya nyumbani kwake kabla ya kuisha kwa eda?

Jibu: Mwanamke mwenye damu ya uzazi hakuna neno kwake kutoka nyumbani kwake. Asipokuwa na haja basi bora kwa wanawake wote kulazimiana na majumba. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَى

“Tulizaneni majumbani mwenu na wala msijishauwe kwa kuonyesha mapambo kama walivyojishauwa zama za ujahili.”[1]

[1] 33:33

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 62
  • Imechapishwa: 01/09/2019