Inafaa kwa mwanafunzi kumkufurisha mtu kabla ya wanachuoni?

Swali: Je, inafaa kwa mwanafunzi ambaye ameimarika katika elimu ya Takfiyr akamkufurisha mtu kwa dhati yake pasi na kurejea kwa wanachuoni kutokana na kutegemea kwake ile elimu alionayo?

Jibu: Mambo ya Takfiyr ni ya khatari. Kuna wengi wameteleza katika jambo hili. Katika jambo hilo mtu anatakiwa kurejea kwa wanachuoni. Hahukumiwi yeyote kwamba ni kafiri isipokuwa baada ya mtu huyo kusimamishwa katika mahakama ya kidini ambapo watadurusu yale yanayopelekea katika ukafiri wake kupitia maneno na matendo yake. Baada ya hapo ndio atakufurishwa. Ama kusema kila mmoja akufurishe ni kitu kisichojuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: al-Istiqaamah ´alaa Diynillaah
  • Imechapishwa: 13/03/2021