Inafaa kwa mtu kula katika vichinjwa vya nadhiri yake?

Swali: Kama mtu ataweka nadhiri kwa mfano endapo ataruzukiwa watoto basi atachinja vichinjwa vitatu itafaa kwake kula katika vichinjwa hivyo au ni lazima kwake kuigawanya kikamilifu?

Jibu: Katika hali hii ataulizwa kuhusu nia yake. Wakati fulani mtu anaweka nadhiri aina hii kwa ajili tu ya kuonyesha furaha kama ambavyo mtu anaonyesha furaha kwa kupokea mgeni na akamchinjia kichinjwa. Nadhiri hii hukumu yake ni nadhiri ilioruhusiwa. Kwa msemo mwingine ni kwamba anapewa khiyari baina ya kuitimiza na akala yeye, familia yake, ndugu zake na majirani zake na baina ya kutoa kafara ya yamini. Hii ndio kanuni kuhusu nadhiri ilioruhusiwa; mtu anapewa khiyari kati ya kutimiza kile alichokiwekea nadhiri au kutoa kafara ya yamini. Ama ikiwa hiki alichokiwekea nadhiri kwamba Allaah akimruzuku mtoto basi atachinja kwa mfano kondoo. Ikiwa nia yake ni kuchinja kwa ajili ya kumshukuru Allaah (´Azza wa Jall) juu ya neema hii basi inafuata mkondo wa swadaqah. Hivyo atawalisha nayo mafukara na masikini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (13) http://binothaimeen.net/content/13572
  • Imechapishwa: 03/02/2021