Inafaa kwa mtu ambaye kazi yake ni udereva kufupisha swalah?


Swali: Je, inafaa kwa dereva kufupisha swalah zake safarini?

Jibu: Akiwa na nyumba na nchi anayoishi ndani yake, haitofaa kwake kufupisha. Ama akiwa hana mahali, kama wabaharia wa meli, hakuna neno [wakafupisha]. Kwani yeye hukumu yake ni kama wasafari wengine. Safari haikatiki kwake mpaka pale atapofika kwa familia yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 28/12/2018