Inafaa kwa msafiri kukusanya kati ya ijumaa na ´Aswr? IX


Swali: Tulisafiri kwenda ´Umrah kisha tukakusanya baada ya swalah ya ijumaa katika msikiti Mtakatifu. Je, inajuzu?

Jibu: Haijuzu kukusanya ´Aswr pamoja na swalah ya ijumaa. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا

“Kwani hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.”[1]

Bi maana wakati uliopangwa. Mambo yakishakuwa ni hivo ni kwamba haifai kukusanya kati ya swalah mbili isipokuwa tukijua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo. Haikupokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya ´Aswr pamoja na ijumaa. Hata siku moja. Alikuwa akikusanya ´Aswr pamoja na Dhuhr kwa sababu ni aina yake. Ama swalah ya ijumaa inatofautiana na Dhuhr tofauti kubwa…

Namwambia ndugu huyu muulizaji ni lazima hivi sasa mrudi kuswali ´Aswr Rak´ah nne. Hili ni salama zaidi. Ni salama zaidi kwa njia ya kuswali mbili au nne na si kwa njia ya kuirudi. Kuirudi ´Aswr ni lazima muirudi ima Rak´ah mbili au Rak´ah nne. Mkiswali Rak´ah mbili peke yake hakuna neno kwa sababu msafiri anaswali Rak´ah mbili. Na mkiswali Rak´ah nne hivi sasa, kwa sababu hivi sasa mko katika hali ya ukazi, mfanye hivo.

[1] 04:103

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1387
  • Imechapishwa: 12/07/2019