Swali: Inafaa kwa msafiri kukusanya swalah ya ijumaa na ´Aswr?

Jibu: Swalah ya ijumaa haikusanywi na kitu kingine. Lakini ukiiswali kwa aina ya Dhuhr itafaa kwako kuiswali Dhuhr na ´Aswr kwa pamoja. Ama ukiiswali kwa aina ya ijumaa usiikusanye pamoja na ´Aswr. Swalah ya ijumaa haikusanywi na kitu kingine. Ukifika wakati wa ´Aswr inafaa kuswali Rak´ah mbili. Aliyeswali ´Aswr pamoja na swalah ya ijumaa kwa ujinga basi ni lazima kwake kuirudi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 13/04/2019