Inafaa kwa msafiri kukusanya kati ya ijumaa na ´Aswr? II


Swali: Mtu akiwa njiani afupishe swalah ya ijumaa au aiswali Rakaa´ nne kwa sababu tumesikia kutoka kwako ya kwamba haijuzu kwa mtu kufupisha swalah ya ijumaa wala kuijumuisha pamoja na ´Aswr? Ni upi sahihi wa nukuu hii?

Jibu: Nukuu kwa sura kama hii ni uongo na mimi sijasema maneno haya.

Kuhusu kwamba ijumaa haifupishwi ni kweli. Ijumaa ikifupishwa itakuwa Rakaa´ moja tu, jambo ambalo halikusemwa na mwanachuoni yeyote wala hakuna hata mjinga anayesema hivo. Ijumaa haifupishwi. Inaswaliwa vilevile Rakaa´ mbili. Msafiri akipita katika mji siku ya ijumaa na akatua hapo na akasema kuwa ataendelea na safari yake jioni na swalah ya ijumaa ikamkuta hapo, haifai akaijumuisha pamoja na ´Aswr. Ijumaa ni swalah ya kipekee, ilio na masharti maalum na sifa maalum. Sunnah imekuja kujumuisha kati ya Dhuhr na ´Aswr ambapo ijumaa sio Dhuhr. Kwa ajili hii si sawa kujumuisha ijumaa na ´Aswr. Ambaye alijumuisha ijumaa na ´Aswr tunamwambia arudi kuswali ´Aswr Rakaa´ mbili baada ya kuingia wakati wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (25)
  • Imechapishwa: 18/01/2019