Inafaa kwa msafiri aliyetua katika mji kufupisha na kukusanya swalah?


Swali: Inajuzu kwa mwanamke msafiri anapotua kwenye nyumba kuswali kwa kufupisha na kukusanya au ni lazima kuswali kila swalah kwa wakati wake?

Jibu: Kumeshatangulia swali kama hili na tumesema kuwa inafaa kwa msafiri kufupisha swalah zake midhali bado ni msafiri mpaka pale ataporudi katika mji wake. Ataposafiri mwanamke na akatua kwenye mji kwa muda wa siku mbili, tatu, nne, siku kumi au zaidi ya hapo na yeye nia yake ni kurudi katika mji wake, basi katika hali hii inafaa kwake kufupisha swalah. Kwa kuwa ni msafiri. Lakini asikusanye swalah isipokuwa kwa kuhitajia hilo. Tumesema kuwa kukusanya swalah safarini sio Sunnah isipokuwa kwa yule ambaye anahitajia hilo. Ikiwa katika mji huo aliotua hahitajii kukusanya basi lililo bora ni yeye kutozikusanya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/726
  • Imechapishwa: 26/11/2017