Inafaa kwa baba kuchukua katika mali ya mtoto wake?


Swali: Je, baba anaweza kuchukua kitu kutoka katika mshahara wa mtoto wake? Akimuombea du´aa dhidi yake itakubaliwa?

Jibu: Ndio. Inafaa kwake kuchukua kitu kutoka katika mali ya mtoto wake. Inafaa kwake kufanya hivo kwa masharti mawili:

Ya kwanza: Asimdhuru. Akachukua kilicho zaidi ya haja yake.

Ya pili: Baba asimpe mtoto wake mwingine.

Kwa ajili hii wakati mwanamume mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Baba yangu anataka kuchukua pesa zangu.” Ndipo akasema: “Wewe na mali zako ni milki ya baba yako.”

Baba ana haki ya kuchukua sehemu kutoka katika mali za mtoto wake. Ni mamoja akawa mwanamume au mwanamke kilichozidi juu ya haja yake. Endapo atakuwa sio mwenye kuhitajia hapana. Asichukue kile kilichozidi juu ya haja za mvulana au msichana wake. Jengine ni kwamba asimpe mtoto wake mwingine. Akimpa mtoto mwingine itakuwa ni miongoni mwa sababu za kuasiwa. Akichukua kilicho juu ya haja zake kwa njia ya kwamba hamdhuru na wala hampi mtoto mwingine hakuna neno.

Kutokana na haya akiwa ni mwenye kuhitaji na asimpe kitu kunachelea akaingia katika kuwaasi wazazi. Baba akiwa ni muhitaji na akamuomba mtoto wake wakike au wakiume ampe matumizi, basi itakuwa ni wajibu kumhudumia katika hali hii. Akimnyima basi atakuwa amezuia kitu ambacho ni cha wajibu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2018