Inafaa kuwaua makafiri walioko katika kisiwa cha kiarabu?

Swali: Wako ambao wanatoa fatwa juu ya kufaa kuwaua makafiri walioko katika kisiwa cha kiarabu. Hoja yao ni kwamba makafiri hawa hawana mkataba wowote na waislamu kwa sababu nchi zao zinawapiga vita waislamu kwa kutumia jina “ugaidi”.

Jibu: Hizi ni katika fatwa za wajinga na wenye kujifanya wanachuoni. Haijuzu kuwaua makafiri ambao wamekuja kwa mkataba na wameingia kwa amana. Huu ni udanganyifu na khiyana. Haijuzu kufanya hivi japokuwa watakuwa katika kisiwa cha kiarabu. Inafaa kwao kuingia katika kisiwa cha kiarabu kwa ajili ya kubadilishana mambo ya kimanufaa. Ima wakawaja kama wasafiri, wafanya biashara au wafanya kazi ambao wamekuja kufanya kazi ambazo hakuna wengine wanaozimairi zaidi yao. Haya yanafaa. Kilichokatazwa ni kuwaacha makafiri wakafanya makazi ya kudumu katika kisiwa cha kiarabu. Ama wao kuingia katika kisiwa cha kiarabu kwa ajili ya biashara kisha baadaye watatoka, ni jambo ambalo halina ubaya.

Isitoshe jengine ni kwamba yule ambaye anawatoa makafiri na kuwazuia wasifanye makazi ya kudumu katika kisiwa cha kiarabu ni mtawala. Hio sio haki ya kila mmoja. Anayezungumzishwa ni mtawala wa waislamu. Wanatakiwa kuwaondosha wakiweza kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidhl-il-Islaam (08) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/08.mp3
  • Imechapishwa: 16/02/2019