Inafaa kuwatii wazazi wasiotaka watoto kufunga kwa ajili ya masomo?


Swali: Je, mitihani ya shuleni ni udhuru unaomruhusu mtu kula katika Ramadhaan? Kwa sababu kumeenea kati yetu baadhi ya fataawaa zinazoruhusu kula katika Ramadhaan kwa yule anayechelea ubongo kutofanya kazi vizuri. Je, inajuzu kuwatii wazazi kwa kula kwa ajili ya kuruhusu fataawaa kama hizi zinazoruhusu kutofunga?

Jibu: Mitihani ya masomo na mfano wake haizingatiwi kuwa ni udhuru unaomruhusu mtu kula mchana wa Ramadhaan. Haijuzu kuwatii wazazi kwa kula kwa ajili ya mtihani. Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi muumba. Utiifu unakuwa katika mema pekee. Hivyo ndivyo ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/241)
  • Imechapishwa: 10/06/2017