Inafaa kuwapa Zakaat-ul-Fitwr makafiri?


Swali: Kuna watu wengi walio na wafanya kazi makafiri nyumbani. Je, wawatolee Zakaat-ul-Fitwr au wawape kitu zakaah?

Jibu: Haijuzu kuwatolea Zakaat-ul-Fitwr na wala haijuzu kuwapa kitu katika zakaah. Lau atawapa kitu katika zakaah si sahihi. Lakini anaweza kufanyia wema pasi na zakaah iliyofaradhishwa pamoja na kujua ya kwamba bora zaidi ni mtu kujitosheleza nao na badala yake achukue walio waislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameacha anausia kuwaondosha makafiri katika kisiwa cha kiarabu na akasema:

“Kusikusanyike ndani yake dini mbili.”[1]

[1] Ahmad (06/274).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/375)
  • Imechapishwa: 23/06/2017