Inafaa kuwaoa wanawake wa kinaswara wenye imani ya utatu?

Swali: Inafaa kumuoa mwanamke wa kinaswara, pamoja na kuwa ni mshirikina anayeamini imani ya kumfanya Allaah kuwa na utatu na shirki nyenginezo? Je, hukumu yake ni kama waabudu mizimu au anaingia katika aina nyingine?

Jibu: Allaah amehalalisha hili. Walikuwa wakisema hivi wakati ambapo Qur-aan inateremshwa. Allaah amehalalisha hili. Yeye (Subhaanah) pekee ndiye Mwenye kuhukumu na ndiye mtambuzi zaidi juu ya manufaa ya waja Wake. Hili tumekhafifishiwa. Amesema (Ta´ala):

يَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ

“Leo mmehalalishiwa vizuri na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao na wanawake watwaharifu katika wale waumini wanawake na wanawake watwaharifu katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu.” (05:05)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/03.mp3
  • Imechapishwa: 12/10/2018