Swali: Ni jambo linalotambulika kwamba kuwaoa wanawake wa kiyahudi na wa kinaswara ni jambo linalojuzu. Lakini baadhi ya wanachuoni hii leo wamelikataza jambo hilo kwa hoja kwamba wamekuwa washirikina, wanamwabudu na kumuomba al-Masiyh badala ya Allaah. Baadhi yao hawashikamani na dini yao ya haramu. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Msingi ni kubaki yaliyokuweko kama yalivyokuwa. Ambaye alikuwa mnaswara akiamini dini ya unaswara na anajinasibisha na dini ya unaswara na wakati huohuo akawa anatambulika kuwa ni mwenye kuchunga heshima yake na si mtundu, basi itafaa kumuoa. Kwa sababu Allaah ametaja wanawake wenye kujichunga na uzinzi. Hata hivyo bora ni kuacha kufanya hivo. Ndio maana ´Umar na kikosi cha Maswahabah wengine wameonelea hilo kuchukiza kwa kuchelea juu ya waislamu wasije kuvutwa kwenye unaswara wao au wana wao. Ikiwa hali ilikuwa namna hii wakati wa ´Umar tusemeje zama zetu? Khatari ni kubwa. Mtu anatakiwa asimuoe kabisa. Kwa sababu, ijapokuwa ni kitu kimehalalishwa, lakini shari yake ni kubwa kutokana na uchafu wao na unyonge wa imani ya waislamu mara nyingi. Isitoshe jengine hili lina khatari juu yake na juu ya kizazi chake. Salama na bora zaidi kwake asimuoe kabisa kutokana na ile khatari kubwa inayopatikana kwa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4826/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 27/11/2020