Swali: Ni lini imekokotezwa zaidi kutumia Siwaak? Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak wakati wa Khutbah?

Jibu: Imekokotezwa zaidi kutumia Siwaak wakati mtu anapoamka kutoka usingizini, mara ya kwanza mtu anapotaka kuingia nyumbani, wakati wa kutawadha katika kusukutua na mtu anaposimama kwa ajili ya kuswali.

Ni sawa kwa yule mwenye kusubiri swalah kutumia Siwaak. Lakini asitumie Siwaak wakati wa Khutbah. Kwani kufanya hivo kunamshughulisha. Isipokuwa ikiwa kama atakuwa na miayo. Katika hali hii atumie Siwaak ili kufukuza usingizi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/115)
  • Imechapishwa: 16/06/2017