Inafaa kutoa rushwa ili kuajiriwa ikiwa hakuna njia nyingine?


Swali: Je, inajuzu kwangu kutoa kiwango fulani cha pesa ili kuajiriwa kwangu kuweza kutimia pamoja na kuzingatia kwamba kupata kazi katika nchi yangu hakutimii isipokuwa kwa njia kama hii?

Jibu: Hapana. Hii ni rushwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwenye kutoa rushwa na yule mwenye kupokea. Ni haramu isiyojuzu. Milango ya riziki imefunguliwa. Tafuta riziki:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yule anayemcha Allaah humjaalia njia [ya kutokea] na atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.”[1]

Riziki haipatikani kwa kuajiriwa peke yake.

[1] 65:02-03

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (49)
  • Imechapishwa: 29/01/2022