Swali: Ni ipi hukumu ya kuadhini kwenye sikio la maiti na kumlakinia “Laa ilaaha Allaah” na kumwambia atayowajibu Malaika wawili baada ya kuzikwa?

Jibu: Kutoa adhaana kwenye sikio la maiti ni Bid´ah. Kumlanikia shahaadah ni jambo limeamrishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kuhusu kumwambia majibu atayowajibu Malaika wawili baada ya kuzikwa ni jambo limepokelewa katika Hadiyth. Lakini hata hivyo ni Hadiyth dhaifu isiyotakiwa kutegemewa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/73-74)
  • Imechapishwa: 17/06/2017