Inafaa kusikiliza nyimbo za wanawake siku ya harusi?

Swali: Unasemaje kwa mwenye kusema kuwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amewajuzishia wanaume kusikiliza nyimbo za wanawake wanapopiga dufu?

Jibu: Hili wamelijuzisha wanachuoni wengi katika mnasaba wa ndoa tu [wanawake kuimba]. Katika mnasaba wa ndoa wanawake wanaimba wao kwa wao nyimbo zenye kujulikana ambazo hazina mdundiko, muziki na ala za muziki. Jambo lingine ni kwamba zinakuwa nafasi maalum kwa wanawake peke yao ambapo wanaume hawawezi kuzisikia. Kwa kuwa sauti ya mwanamke ni ´Awrah inayowafitinisha watu. Hili linakuwa kati ya wanawake tu wao wenyewe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-07-18.mp3
  • Imechapishwa: 09/08/2020