Inafaa kusherehekea sikukuu zilizofanywa kama desturi?

Desturi hii ni desturi ambayo ni batili. Inazingatiwa kuwa ni uzushi. Kila uzushi ni Motoni. Kwa hivyo ni lazima kuiacha na kutoifanya.

Ikiwa mtu atahoji kwamba hii ni desturi tu na msingi katika desturi ni uhalali, tutasema kwamba watu hawa wao wameifanya siku hii kuwa ni sukukuu na wameweka ndani yake yale ambayo hayakuwekwa na Allaah (´Azza wa Jall) wala Mtume Wake. Kuhusiana na mambo ya sikukuu Uislamu haukuweka sikukuu yoyote zaidi ya ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhwhaa na sikukuu ya wiki ambayo ni siku ya ijumaa.  Mbali na hizo miongoni mwa zile ambazo watu wamefanya kuwa ni sikukuu na desturi zinazokwenda kinyume na Shari´ah ni batili.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ul-Waduud (01/37) http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=16365
  • Imechapishwa: 19/12/2019