Inafaa kusema Muhammad ndiye mpenzi wangu?


Swali: Inajuzu kwa mtu kusema:

“Allaah ndiye mpenzi na khaliyliy wangu?”

Jibu: Sijui chochote juu ya hilo. Sema Allaah ndiye Mola wangu na mimi ndiye mja wake.

Swali: Inajuzu kwa mtu kusema kwamba khaliyliy wake ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Ni sawa. Hakuna neno. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) alisema:

“Khaliyliy wangu aliniusia… “

Akimaanisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (74) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-25-01-1439H-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2017