Inafaa kusema “fulani ni walii wa Allaah?”

Swali: Inajuzu kusema juu ya mtu ambaye amefikia kiasi kikubwa cha elimu na uchaji Allaah:

“Mtu huyu ni walii wa Allaah?”

Jibu: Sisi hatushuhudii na wala hatumkatii yeyote isipokuwa yule aliyeshahidiliwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Miongoni mwa misingi ya ´Aqiydah ni kwamba sisi hatumshahidilii yeyote uwalii wala Pepo kama ambavyo vilevile hatumkatii yeyote Moto. Isipokuwa yule aliyeshahidiliwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hata hivyo tuna matarajio kwa mtu mwema na tunachelea kwa muovu. Huu ni msingi katika ´Aqiydah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 18/11/2016