Swali: Mara nyingi nawaona baadhi ya waswaliji wakipangusa juu ya soksi zao wakati wa kutawadha mpaka katika wakati wa majira ya joto. Naomba kupewa faida kufaa kufanya hivo. Ni lipi bora kwa mkazi wakati anapotawadha kuosha mguu au kupangusa juu ya soksi? Wale wanaopangusa hawana udhuru zaidi ya kusema kwamba kitendo hicho kimeruhusiwa.

Jibu: Ujumla wa Hadiyth Swahiyh zinajulisha kufaa kupangusa juu ya soksi wakati wa majira ya baridi na wakati wa majira ya joto. Sitambui dalili ya ki-Shari´ah inayofanya umaalum wa kupangusa wakati wa majira ya baridi peke yake. Lakini haifai kwake kupangusa juu ya kile kinachofunika mguu isipokuwa kwa sharti zinazozingatiwa na Shari´ah. Miongoni mwazo ni kama ifuatavyo:

1 – Kile kinachofunika mguu kiwe kimefunika yale maeneo ambayo ni lazima kuoshwa.

2 – Awe ameivaa akiwa na twahara.

3 – Kuzingatia muda ambao ni mchana mmoja na usiku wake kwa ambaye ni mwenyeji na michana mitatu na nyusiku zake kwa ambaye ni msafiri.

Muda huu unaanza kuhesabiwa kuanzia mpanguso wa kwanza baada ya kupatwa na hadathi kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/113)
  • Imechapishwa: 16/08/2021