Inafaa kunywa maji wakati wa swalah ya Sunnah?

Swali: Ni kweli kwamba inajuzu kunywa maji wakati mtu anaswali swalah ya Sunnah?

Jibu: Imepokelewa kutoka kwa Ibn-uz-Zubayr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) katika mnasaba wa swalah ya usiku. Anarefusha swalah ya usiku ambapo anahitajia kunywa maji wakati wa swalah. Hili limepokelewa kwa mnasaba wa swalah ya Sunnah na sio swalah ya faradhi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20maji%20d%20-%2011%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017