Inafaa Mume Kumwita Mamake Mke “Mama”?


Swali: Katika desturi zenu mtu humwita mama mkwe wake “Mama”. Je, wito huu unajuzu?

Jibu: Hapana. Imechukizwa kufanya hivi. Ni machukizo yaliyopendekezwa. Asimwambie mke wake “Mama” au “Dada” kwa sababu inafanana na Dhwihaar. Vilevile asimwambie mama mkwe wake “Mama” kwa kuwa akiwa ni mama yake basi msichana wake atakuwa ni haramu kwake. Imechukizwa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (03) http://alfawzan.af.org.sa/node/2046
  • Imechapishwa: 23/10/2016