Inafaa kumuuzia kafiri kitu cha haramu kama TV au dishi?

Swali: Mtu huyu aliyetubia kutokamana na dishi alikuwa ni mwenye kuhitaji pesa. Je, anaweza kumuuzia mnaswara?

Jibu: Mimi nanyamaza juu ya hili. Mtu kuuza bidhaa za haramu kwa makafiri inafaa? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliharamisha kuuza pombe. Tokea wakati huo ikawa ni haramu kuwauzia waislamu na wasiokuwa waislamu. Kadhalika wakati ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) alipoandikiwa barua kwamba waabudu moto au manaswara wanataka kuwapa waislamu kitu katika pombe, ´Umar akawakataza na akawaambia wasipokee. Waacheni wao wauziane wao kwa wao na chukueni katika thamani yake. Kwa hali yoyote mimi nanyamaza juu ya jambo hili. Namwambia: mtegemee Allaah, ivunje na nakubashiria kheri yenye kuja haraka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/788
  • Imechapishwa: 20/01/2018