Inafaa kumuasi mzazi asiyetaka mwanae kwenda msikitini kufanya I´tikaaf?

Swali: Ni ipi hukumu mzazi asipompa ruhusa mtoto wake kwa sababu zisizokinaisha?

Jibu: I´tikaaf ni Sunnah. Kuwatii wazazi ni wajibu. Sunnah haiwezi kuiangusha wala kuipinga wajibu. Wajibu ni yenye kutangulia mbele yake. Allaah (Ta´ala) amesema katika Hadiyth al-Qudsiy:

ما تقرب إليَّ عبدي بشيء أحب إليّ مما افترضت عليه

“Mja hatojikurubisha Kwangu kwa kitu kinachopendwa zaidi kwangu kuliko yale niliyomfaradhishia.”

Ikiwa baba yako amekuamrisha kuacha kufanya I´tikaaf na kukutajia sababu basi hiyo inapelekea wewe kuacha kufanya hivo. Yeye ni mwenye kukuhitajia. Yeye ndiye mwenye mizani na si wewe. Mizani kwa mujibu wako inaweza kuwa sio ya sawa na sio ya uadilifu kwa kuwa wewe unatamani kufanya I´tikaaf. Matokeo yake ukaona kuwa hoja hizi sio sababu ilihali baba yako anaona kuwa ni sababu. Kwa hivyo mimi nakunasihi usifanye I´tikaaf. Lakini asipokutajia sababu za kueleweka juu ya hilo katika hali hii haitokulazimu kumtii. Kwa sababu haikulazimu kumtii katika jambo ambalo halina manufaa upande wake na wakati huo huo lina manufaa kwako.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/159)
  • Imechapishwa: 15/06/2017