Inafaa kumsalimia muislamu ´as-Salaam ´alaa manit-Taba´ al-Hudaa”?

Swali: Ni ipi hukumu ya kumsalimia muislamu kwa kusema:

السلام على من اتبع الهدى

“Amani iwe juu ya yule mwenye kufuata uongofu?”

Muislamu asalimie vipi waislamu waliokusanyika sehemu moja na makafiri?

Jibu: Haijuzu kwa mtu kumsalimia muislamu mwenzie kwa kusema ´as-Salaam ´alaa manit-Taba´ al-Hudaa”. Kwa kuwa formula hii aliisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipowaandikia wasiokuwa waislamu. Muislamu mwenzie mwambie:

السلام عليكم

“Amani iwe juu yenu.”

Ama kusema ´as-Salaam ´alaa manit-Taba´ al-Hudaa” hiyo inapelekea mtu kufahamu kuwa ndugu yako huyu sio katika wanaofuata uongofu.

Ikiwa waislamu wamekusanyika sehemu moja na manaswara, basi awasalimie salamu ya kawaida kwa kusema:

السلام عليكم

“Amani iwe juu yenu”

na huku akiwakusudia wale waislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/35)
  • Imechapishwa: 06/06/2017