Inafaa kumpachika mtu ukafiri atapotenda ukafiri?

Swali: Inajuzu kumpachika ukafiri mtu kwa dhati yake pale atapofanya kitendo chenye kukufurisha?

Jibu: Yatapotimia masharti ya Takfiyr kwake basi itafaa kumpachika ukafiri kwa dhati yake. Katika hali hiyo atatakiwa kutaamiliwa kama kafiri kwa kuzingatia hukumu za hapa duniani. Kuhusu hukumu za Aakhirah unatakiwa kusema kwa ujumla na sio mtu kwa dhati yake. Kwa ajili hiyo ndio maana Ahl-us-Sunnah wakasema:

“Hatumkatii yeyote si Pepo wala Moto isipokuwa tu yule aliyeshuhudiwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Vivyo hivyo tunasema:

“Atakayefunga Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio basi atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia na yatayokuja huko mbele.”[1]

Lakini hata hivyo hatumkatii haya mtu kwa dhati yake. Kwa sababu hukumu iliyofungamana na sifa fulani haipachikwi kwa watu isipokuwa kwa kupatikana masharti ya upachikaji huo na kutokuwepo vikwazo.

[1] al-Bukhaariy (1901) na (2014) na Muslim (760).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/125)
  • Imechapishwa: 25/07/2017