Swali: Je, inajuzu kuwapa zakaah baadhi ya watu ambao wana maasi ya waziwazi kama kwa mfano kifaa cha dishi pamoja na kuwa wanahitajia sana?

Jibu: Ndio, inafaa kuwapa. Lakini hata hivyo inatakiwa kuweka mwakilishi pindi mtu atapochelea kuwa wataitumia katika maasi. Katika hali hiyo mtu amuombe yule baba mwenye nyumba aweke mwakilishi. Baada ya hapo mtu ampe zakaah mwakilishi yule aweze kuwanunulia vile vitu wanavyohitajia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 30/11/2018