Inafaa kumjamii mwanamke mwenye damu ya ugonjwa

Swali: Mwanamke mwenye damu ya ugonjwa anahalalika kwa mume wake?

Jibu: Mwanamke mwenye damu ya ugonjwa ni yule ambaye anayo damu ambayo si hedhi wala damu ya uzazi. Hukumu yake ni wanawake waliosafika. Hivyo atafunga, ataswali na atahalalika kwa mume wake. Atatakiwa kutawadha juu ya kila swalah kama mfano wa wale watu wenye hadathi endelevu inayotokana na mkojo, upepo au kitu kingine. Aidha anapaswa kujihifadhi kutokamana na damu kwa pamba au kitu kingine ili asichafue mwili na nguo yake. Hivo ndivo zilivyosihi Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/213)
  • Imechapishwa: 05/09/2021