Inafaa kukodisha mwanamke wa kupiga dufu harusini?        

Swali: Ikiwa kupiga dufu [katika ndoa] ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Je, inajuzu kukodisha wanawake wapiga dufu?

Jibu: Ndio, inajuzu kukodisha wanawake wapiga dufu. Kwa sababu hiki ni kitendo kilichoruhusiwa, bali ni kitendo kilichowekwa katika Shari´ah. Kila kitu ambacho kitakuwa kinajuzu au kimewekwa katika Shari´ah ni halali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anapoharamisha kitu, basi vilevile huharamisha thamani yake.”

Chukua kutoka kwenye Hadiyth hii kanuni mbili:

1- Allaah akiharamisha kitu basi huharamisha vilevile thamani yake.

2- Allaah akihalalisha kitu basi huhalalisha vilevile thamani yake.

Kujengea juu ya haya inafaa kukodisha mwanamke mwenye kupiga dufu. Lakini ni lazima kukodisha huku iwe ni kitu kinachoingia akilini, ninamaanisha ule mshahara wake uwe unaingia akili. Si sawa kwa mfano kumpa 5.000 (takriban 2.920.925 TZS) kwa ajili ya kupiga dufu saa moja au saa mbili. Huu ni ubadhirifu na israfu. Ikiwa mwanamke hawezi kuja kuimba isipokuwa kwa kupokea 5.000 kwa saa moja au mbili, usifanye hivo. Tayarisha 500 na utapata muimbaji hata kama nyimbo haitokuwa kama nyimbo ya yule ambaye anajulikana. Inatosheleza kile kichache atachoimba. Pesa zenye kubaki 4.500 watumie ndugu zako waislamu katika miji ya Kiislamu na vilevile ndugu zako wengine wahitaji katika miji ya Kiislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
  • Imechapishwa: 03/05/2020