Inafaa kuchana nywele katika masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah?

Swali: Inajuzu kwa mwanamke kuchana nywele zake katika masiku kumi ya Dhul-Hijjah?

Jibu: Ikiwa hatochinja hakuna neno. Ama ikiwa atachinja inafaa kwake kuchana lakini asizikate nywele zake. Achane na kuzitengeneza lakini asikate. Hapa ni pale ambapo kama atachinja. Lakini ikiwa hatochinja inafaa kwake na himdi zote anastahiki Allaah. Lakini kuzichanua na kuzitengeneza hakuna ubaya japokuwa atachinja. Hata hivyo asikudie kukata nywele. Ni mamoja awe atachinja kwa ajili yake mwenyewe, kwa ajili ya wazazi wake au kwa ajili ya mume wake. Sunnah ni yeye kuchinja kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wa nyumbani kwake. Wajumuike wote [katika kichinjwa hicho] kwa ajili yake mwenyewe, wazazi wake, mume wake na watoto wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10180/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D8%B4%D8%B7-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D8%B4%D8%B9%D8%B1%D9%87%D8%A7-%D9%81%D9%8A-%D8%B9%D8%B4%D8%B1-%D8%B0%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%AC%D8%A9
  • Imechapishwa: 14/08/2018