Imependekezwa kula safarini ijapokuwa mtu hatohisi uzito wa safari


Swali: Sisi tuko na imamu wa chuo kikuu ambaye anawakariria watu akiwaabia: “Yule mwenye kusafiri katika Ramadhaan na akaacha kufunga basi anapata thawabu mara mbili; thawabu kwa kutendea kazi ruhusa na thawabu za kulipa.” Je, kuna Hadiyth juu ya maudhui haya? Allaah akujaze kheri.

Jibu. Mwenye kugonjweka au akasafiri basi inafaa kwake yeye kuacha kufunga. Bali imependekezwa kwake kufanya hivo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.” (02:185)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anapenda zitendewe kazi ruhusa Zake kama anavochukia kuendewa maasi Yake.”

Kwa sharti iwe ni maradhi yenye kumtia yeye uzito kufunga. Ama ikiwa hayamtii uzito basi haifai kwake kuacha kufunga. Kwani hazingatiwi ni mwenye kupewa udhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/234-235 )
  • Imechapishwa: 24/05/2018