Imechukizwa kuswali swalah ya ´Iyd msikitini


Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali swalah ya ´Iyd ndani ya msikiti?

Jibu: Imechukizwa kuswali swalah ya ´Iyd ndani ya msikiti. Isipokuwa kukiwepo udhuru. Sunnah ni kuswali swalah ya ´Iyd jangwani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali jangwani. Lau kutoka ingelikuwa si lengo asingefanya hivo na wala asingewatia watu uzito kufanya hivo. Isitoshe kuswali ndani ya msikiti jambo la kudhihirisha na kuiweka wazi nembo hii linakosekana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/230)
  • Imechapishwa: 14/06/2018