Swali: Tumewasikia baadhi ya wanafunzi wakisema kuwa ni bora mtu kutosema pindi anapotunga vitabu:

“Imeandikwa na fakiri wa Allaah fulani.”

Hoja yao ni kwamba huku ni kujifananisha na Suufiyyah. Maneno haya ni sahihi?

Jibu: Hapana, si sahihi. Huku ni mtu kukiri uhitaji wake kwa Allaah (´Azza wa Jall). Unataka aandike:

“Imeandikwa na walii wa Allaah fulani”?

Hapana. Huku ni mtu kukiri ufakiri wake na ni kunyenyekea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2053
  • Imechapishwa: 21/01/2017