Imani kwa mujibu wa Khawaarij na Mu´tazilah

Swali: Ni ipi imani kwa mujibu wa Khawaarij?

Jibu: Khawaarij na Mu´tazilah wanaonelea kuwa imani inakuwa kwa moyo, kutamka na kwa viungo vya mwili kama wanavyoamini Ahl-us-Sunnah. Lakini wanaamini kuwa imani kitu kimoja kisichozidi wala kupungua. Ima iwepo yote au itokomee yote. Mtu akifanya maasi makubwa imani yake yote inaondoka tofauti na wanavyoonelea Ahl-us-Sunnah. Ahl-us-Sunnah wanaonelea kuwa mtu akifanya maasi imani yake inashuka na kudhoofika. Lakini hata hivyo imani yake haitoweki yote.

Khawaarij wanakufurisha kwa maasi. Wanaonelea kuwa mwenye kufanya dhambi kubwa anakufuru na imani yake inatoweka. Wanaonelea kuwa mtu kama huyu atadumishwa Motoni milele.

Mu´tazilah  wanaonelea kuwa mwenye kufanya dhambi kubwa ametoka katika imani na wala haingii katika ukafiri kwa hapa duniani. Kwa msemo mwingine wanaonelea kuwa anakuwa katika ngazi kati ya ngazi mbili. Lakini huko Aakhirah wanaafikiana na Khawaarij ya kwamba atadumishwa Motoni milele. Hili ni batili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=67832&audiotype=lectures&browseby=speaker§
  • Imechapishwa: 26/08/2017