Imamu kuwafahamisha waswaliji kama jeneza ni la kiume au la kike

Swali: Punde tu tumeswalia jeneza. Tatizo ni kwamba tulikuwa katika safu za nyuma na hatukujua kuwa ni jeneza na wanawake hawakujua ni kwa nini kunasemwa “Allaahu Akbar” nyingi. Je, kuna ubaya imamu akitangazia kuhusu jeneza na kama ni mvulana au msichana?

Jibu: Hakuna neno katika hali. Kwa msemo mwingine ni kwamba ni sawa imamu akawaambia kwamba wamswalie mwanaume au mwanamke. Lakini kwa mfano wa nyusiku zetu kama hizi haifichikani kwa yeyote kwamba kuna jeneza. Kwa nini? Mkusanyiko mkubwa. Mkusanyiko mkubwa unamfahamisha mtu kwamba kuna jeneza. Jengine ni kwamba imamu anaposimama, akasema “Allaahu Akbar”, baada ya Tasbiyh na Tahliyl akiweza kufanya hivo, itatambulika kuwa ni jeneza. Msingi wa kuzindua kwamba kuna jeneza hakuna ubaya. Lakini mtu afanye hivo wakati wa haja. Ama kukiwa hakuna haja basi haihitajiki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1215
  • Imechapishwa: 26/08/2019