Imamu kuswali maeneo ya juu zaidi kuliko maamuma wake

Swali: Je, inafaa wakati wa kuswali imamu awe maeneo ya juu zaidi kuliko maamuma? Nakusudia Mihraam iko sehemu ya juu kuliko maeneo mengine ya msikiti.

Jibu: Hapana neno kufanya hivo ikiwa ujuu huo ni kidogo. Kwa sababu Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku moja aliwahi kuswali juu ya mimbari, kisha akateremka na akasujudu na akasema baada ya salamu:

“Nimefanya hivo ili mnifuate na mjifunze swalah yangu.”

Kuna maafikiano juu yake.

Vivyo hivyo inafaaa kwa hali zote akiwa yuko na baadhi ya maamuma. Kwa sababu wakati mwingine haja inaweza kupelekea kufanya hivo kwa wingi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/95)
  • Imechapishwa: 21/11/2021